Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) chini ya Umoja wa Mataifa limekuwa likitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa takribani miaka mitatu. Siku kadhaa zilizopita ziliripotiwa taarifa za kulituhumu jeshi hilo kuhusika na unyanyasaji wa kijinsia unaodaiwa kufanywa kwa wananchi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
April 08
2016 kutoka makao makuu ya Jeshi hilo wametoa taarifa za kusikitishwa na
tuhuma hizo na hapa Afisa Habari wa Jeshi hilo James Macheta, ameyazungumza haya….>>>’Jeshi
letu haliwezi kupuuza taarifa hizo, hivyo limeanza kuchukua hatua za
kiuchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo ingawa rekodi za majukumu
ya ulinzi wa amani zilizokwishafanywa na jeshi letu zinaonyesha hakukuwa
na tuhuma kama hizo’;-James Macheta
>>>’Jeshi
letu halitasita kuchukua hatua kali kwa wakaobainika katika tuhuma
hizo, jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania bado lipo imara na
linaendelea kutekeleza majukumu yake nchini Congo kwa kufuata sheria na
utaratibu wa Umoja wa Mataifa‘:-James Macheta
0 comments:
Post a Comment