Kwa Selena Gomez kusikika mwaka 2014 kuwa alienda rehab, wengi walikuwa na imani kuwa huenda ni sababu ya matumizi mabaya ya vilevi – haikuwa hivyo.
Alienda rehab kwasababu alipatikana na ugonjwa uitwao lupus.
“Niligundulika nina lupus. Mama yangu alipata miscarriage ya mapema. Hivyo ilibidi nisitishe ziara yangu. Nilihitaji muda kuwa sawa,” ameliambia jarida la GQ.
Na kile kitendo cha watu kuendelea kumuuliza kuhusu rehab ikiwa ni miaka miwili imepita tayari, kinaonesha kuanza kumkera.
“Inachanganya sababu kwa asilimia 100 ninaruhusiwa kuwa na hivyo. Sidhani kama ina maana sana. Mambo yangu ya zamani yanaonekana kuwafurahisha zaidi watu kuliko mustakabali wangu kitu kinachonikera.”
0 comments:
Post a Comment