RIYAD MAHREZ ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA PFA


Mshambuliaji wa Leicester City, Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya Chama cha Wachezaji wa Kulipwa Uingereza (PFA) kwa kuchaguliwa mchezaji bora wa mwaka.

Mahrez amefunga magoli 17 na kusaidia 11 katika michezo 34 ya Ligi Kuu ya Uingereza na kuchangia Leicester kuelekea kuweza kutwaa kombe la ligi hiyo.

Kiungo wa Tottenham, Dele Alli, 20, alitwaa tuzo ya mchezaji kijana wa kulipwa wa mwaka, huku mshambuliaji wa Manchester City, Izzy Christiansen akitwa tuzo ya mchezaji wa kike bora wa mwaka.
                                      Kiungo wa Tottenham, Dele Alli, akiwa na tuzo yake
            Mshambuliaji wa Manchester City, Izzy Christiansen, akiwa na tuzo yake
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment