Wananchi wa kijiji cha Toraja, huko Sulawesi ya Kusini, nchini
Indonesia, kila baada ya miaka mitatu, hufukua na kusafisha maiti ya
ndugu zao.
Ieleweke kuwa hawafukui maiti hiyo hiyo kila miaka mitatu ila kila maiti
inapozikwa, kwa wale wanafuata utamaduni huu, hufukuliwa mara moja na
kusafishwa na kuzikwa tena. Na sherehe hiyo inafanywa kila miaka mitatu
katika mwezi wa Nane.
Sherehe hiyo inaitwa Ma'nene na wananchi wa kijiji hicho wanaamini kuwa
kufanya hivyo inawaletea baraka kwa kuwakumbuka marehemu na kuwasafisha
na kuwavalisha nguo ili wapendeze na kuwabariki.
Haijulikani imeanza lini hii sherehe na serikali haiingilii zoezi hili kulinda utamaduni wa watu wa kijiji hiki.
0 comments:
Post a Comment