Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Nay wa Mitego alisema wimbo huo utatoka pamoja na video mpya.
“Shika Adabu Yako, bado inafanya vizuri sana mtaani kusema kweli, lakini mimi ni msanii wa watu wote, kuna mashabiki wanahitaji kazi mpya. Kwa hiyo tarehe 9 mwezi wa 5 naachia wimbo mpya pamoja na video, na tarehe 6.6.16 nitachia wimbo mwingine video na Audio,” alisema Nay.
Aliongeza, “Huu ni ujio mpya wa Nay wa Mitego, ukiangalia ni tofauti na kazi zilizopita ambazo nilikuwa natoa audio na baadae video, lakini sasa hivi sitaki mchezo kila ngoma inatoka na video,”
0 comments:
Post a Comment