Rais wa kwanza wa Zanzibar HayatiSheikh Abeid Amani Karume
Leo April 7, 2016 ni siku ya kumbukumbu ya miaka 44 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi.
Mzee Karume aliongoza nchi baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964.
Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya Muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania, Mzee Karume alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wanafunzi wakitembelea mahali alipouwawa Hayati Mzee Karume.
About Unknown
Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com
Phone:0719337774
0 comments:
Post a Comment