Nyota wa filamu za Bollywood Amitabh Bachchan amekana kuhusishwa na kampuni zozote za kigeni anazotumia kukwepa kulipa ushuru.
India
Express imeripoti kwamba Bw Bachchan aliteuliwa mkurugenzi wa kampuni
nne za kigeni mwaka 1993,zilizosajiliwa katika kisiwa cha Uingereza cha
Virgin Island na Bahamas.Yeye na nyota mwenzake wa kike Aishwarya Rai ni miongoni mwa Wahindi 500 walioorodhshwa katika gazeti la Panama,gazeti hilo limesema.
Mshauri wa Bi Rai wa maswala ya uwanahabari amehoji uhalisia wa ripoti hiyo
Gazeti la India Express liliripoti kwamba bw Bachchan alikuwa amekataa kutoa tamko lolote,lakini alitoa taarifa siku ya Jumanne akikana kujihusisha.
0 comments:
Post a Comment