Alipoulizwa kuchagua kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo nani ndiye anazidi mwingine, Alessandro Del Piero amekubali kuwa kuchagua kati ya hao wa kali duniani ni vigumu sana.
"Sijawahi kujibu swali hili katika maisha yangu kwa sababu ni ngumu sana kwa kuchagua. Wakati huo huo pia ni rahisi sana kuamua. naweza kufumba macho na kuchukua moja ambaye atakuwa bora ila Wote ni wachezaji ajabu, "alisema Del Piero.
Hata Hivyo mwanasoka uyo kongwe wa Juventus ameona kuwa Neymar ana sifa zote zinazohitajika ili kushinda mpira wa Dhahabu.
"Neymar bado ni mchezaji mdogo wakati Messi na Ronaldo ni kama wameanza kufikia mwisho wa kazi zao. Kwa Neymar, ana bahati zote mbele yake na yeye ana nafasi kubwa ya kushinda mpira wa Dhahabu siku moja, " alisema Del Piero.
0 comments:
Post a Comment