Wanaoufatilia muziki wa Hiphop toka kitambo hicho watakumbuka jinsi walivyoruka na hit single ya ‘Lean Back‘ humo ndani wakiwemo Remy Ma na Fat Joe alafu baadae wawili hawa wakagombana kisha Remy Ma akaenda jela kwa miaka sita kwa kisa cha kumpiga mtu risasi baada ya kugundua kaibiwa zaidi ya milioni sita za Kitanzania, akatumikia kifungo chake cha miaka nane kwa miaka sita tu na akaachiwa huru August 2014.
Kuanzia hapo Remy akaingia studio na kuanza kurekodi ngoma, mojawapo ni hii ambayo itawekwa kwenye album ya Fat Joe na Remy Ma  itayotoka baadae mwaka 2016, kwenye mdundo huu wametoa shavu kwa French Montana, Infared.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment