Wiki
kadhaa zimepita tangu Simba 6 walioripotiwa kutoroka kwenye hifadhi ya
wanyamapori ya Nairobi Park na kuonekana wakielekea mji wa Langata.
Leo
March 18 2016 inaripotiwa tena Simba mmoja ametoroka kutoka Hifadhi ya
Taifa ya Nairobi nchini Kenya, ameonekana mtaani na kujeruhi mtu mmoja
asubuhi ya leo.
Polisi wa Kenya wamethibitisha tukio hilo na kusema mtu aliejeruhiwa alifikishwa Hospitali na hali yake inaendelea vizuri. Waangalizi wa Hifadhi wanaendelea na juhudi za kumkamata Mnyama huyo hatari.
0 comments:
Post a Comment