![]() |
Mhandisi wa Ndege akitumia mkebe wa vifaa uliokwisha unganishwa kwenye mfumo mpya mbele ya Ndege ya shirika la Etihad aina ya Airbus A330 ambayo ilikuwa inapitia marekebisho ya kawaida. |
Shirika
la ndege la Etihad kupitia idara yake ya uhandisi limeimarisha uwezo
wake wa matengenezo ya ndege na mfumo mpya wa kujiendesha wenyewe moja
kwa moja (ATC), mfumo ambao unasaidia wahandisi katika upatikanaji,
utunzaji na ufuatiliaji wa vifaa huku ukipunguza uwezekano hatarishi wa
zana kupotea katika mifumo muhimu ya ndege wakati wa matengenezo.
Mfumo
huo ukiwa umeunganishwa na kituo kikuu cha mawasiliano kupitia njia ya
mtandao na hivyo kuuwezesha kukagua zaidi ya matengenezo 15,000
yaliyofanyika, mfumo huu utaweza kutambua vifaa vilivyo potea, kuvunjika
au vilive ambavyo havijarudishwa.
Mkebe
wa vifaa hautoweza kufunguliwa mpaka mhandisi aonyeshe kitambulisho
chake mbele ya kifaa maalumu ha kuhakiki kilichopo mbele ya mkebe huo wa
vifaa. Kitambulisho kitasaidia kuhakikisha mhandisi anamamlaka ya
kutumia vifaa ndani ya mkebe husuika na hivyo mkebe kufunguka. Mkebe huu
wa vifaa unakuja na sehemu ya mhandisi kujaza matengenezo anayotakiwa
kufanya (Idadi/Aina) pamoja na eneo la kazi.
Mfumo
huu mpya ulipitia majaribio yenye mafanikio katika uwanja wa kimataifa
wa ndege wa Abu Dhabi mnamo mwezi Novemba mwaka 2015, na ulikwisha
sambazwa katika vituo vyote vya shirika la ndege la Etihad vya
matengenezo mwezi Januari.
Karibu
wafanyakazi 350 wamepata mafunzo juu ya mfumo mpya, na zaidi ya
matengenezo 50,000 yamekwisha fanyika bila upotevu wa kifaa chochote cha
ufundi.
Jeff
Wilkinson, Makamu wa Rais, Etihad Airways, Ufundi, alisema: "Udhibiti
wa vifaa ni swala muhimu kwa ajili ya mafanikio hasa pale tunapolenga
kuboresha shughuli ya matengenezo ili kupunguza michakato ya kazi,
kuongeza ufanisi na kuimarisha usalama.
"Kupitia
mfumo mpya, wahandisi wetu ni wataweza kumaliza matengenezo haraka na
kwa ufanisi, bila ya kuchukua hatua za ziada kufuatilia, kujiandikisha
au kuangalia walipoacha vifaa wanavyotumia na hivyo kuokoa kwa kiasi
kikubwa muda.”
"Hii
pia huongeza usalama kwani kifaa kilichopotea mikononi mwa mhandisi sio
tu usumbufu bali kinageuka kuwa kifaa hatarishi kwa usalama wa mtu
mwingine” aliongeza
Mfumo
huu unawezesha mikebe yenye vifaa hadi 1,000 mbalimbali ndani yake
pamoja mikebe mingine yenye na vifaa maalumu kwa ajili ya matengenezo ya
umeme na uhandisi wa ndani ya ndege, kupangiwa mhandisi mwenye mamlaka
husika aliyepangiwa kazi maalumu kwenye dege.
Kitengo
cha uhandisi wa matengenezo ya ndege cha Shirika la Ndege la Etihad
hivi sasa kina mikebe 32 ya vifaa vya matengenezo vinavyotumia mfumo huu
mpya ndani yake, kati yake mikebe isiyopungua 20 huwa inatumika kwa
wakati mmoja. Mifumo
iliyobaki itaunganishwa na kituo kikuu na hivyo kuwezesha mifumo hiyo
kama inavyotakiwa ili kukidhi mahitaji ya timu matengenezo kama ndege
inakuja katika kwa ajili ya matengenezo
0 comments:
Post a Comment