Serena amkemea mwandalizi wa Indian Wells

Mchezaji anayeorodheshwa wa kwanza duniani katika tenisi ya wanawake Serena Williams ameshtumu matamshi ya mwandalizi mmoja wa mchezo huo kwamba wachezaji wanawake katika mecho huo wanawategemea sana wanaume.
Raymond Moore aliwaambia waandishi kabla ya siku ya fainali huko India Wells kwamba wanawake wanafaa kupiga magoti na kumshukuru mungu kwa wachezaji kama vile Roger Federer na Rafael Nadal kuwa waliubeba mchezo huo.
Williams alisema matamshi yake yanawatusi wanawake ambao hawana haja ya kumpigia magoti mtu yeyote.
Bwana Moore ambaye pia alizungumzia kuhusu maumbile ya kuvutia ya baadhi ya wachezaji wanawake ameomba msamaha kwa matamshi yake.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment