Paka mwizi wa nguo za ndani za wanaume


Paka mmoja mwizi wakati wa usiku amekuwa akiiba soksi pamoja na nguo za ndani nchini New Zealand.
Katika kipindi cha miezi miwili, paka huyo mwenye umri wa miaka sita kwa jina Brigit kutoka mji wa Hamilton aliiba suruali za ndani 11 na zaidi ya soksi 50.
Mmiliki wake Sarah Nathan alichapisha tabia ya paka huyo isiyo ya kawaida katika mtandao wake wa facebook.
''Tabia hiyo sasa inazidi kuwa mbaya.Lazima kuna mtu ambaye anakosa vitu vyake'',alisema katika chapisho lake la ukursa wa facebook lililosambazwa mara 500.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment