Saa 24 tu tangu kupatikana kwa habari kwamba, ndoa ya staa
wa sinema za Bongo, Wastara Juma aliyoifunga na Mbunge wa Jimbo la
Donge, Zanzibar, Sadifa Juma imevunjika, sasa siri 5 za kuparaganyika
kwa ndoa hiyo ziko mikononi mwa gazeti hili.
Ndoa hiyo ilidaiwa
kuvunjika rasmi Machi 21, mwaka huu baada ya kuishi kwa siku 61 tangu
kufungwa kwake, Januari 8, mwaka huu huko Tabata jijini Dar.
SIRI YA KWANZA
Kwa mujibu wa chanzo chetu kimoja, miongoni mwa siri hizo zilizoisukuma
ndoa hiyo kuvunjika ni kitendo cha Wastara kuomba kila kukicha kwamba,
aachike baada ya madai kwamba, hakukuta furaha kama alivyotegemea.
“Wastara alitegemea kwamba baada ya kuolewa angekuta furaha. Lakini
anavyosema jambo hilo silo alilokumbana nalo ndani ya ndoa. Hiyo ni siri
moja wapo, ikamfanya Wastara amuombe Mungu kila siku ili aachike,”
kilisema chanzo hicho.
SIRI YA PILI
Chanzo kiliendelea kudai kuwa, pia Wastara aliingia kwenye ndoa hiyo
huku moyo wake wote ukibaki kwa mchumba wake wa zamani, Bond Suleiman.
“Wastara tangu akiwa ndani ya maamuzi ya akubali au akatae kufunga ndoa
na Sadifa, alikuwa akisema moyo wake umeelekea sana kwa Bond.
“Hivyo naamini kuwa, hata alipoambiwa anapewa talaka aliipokea kwa
mikono miwili ili arudi kwa Bond. Mimi naamini hivyo,” kilisema chanzo.
WASTARA MWENYEWE NA SIRI NYINGINE
Akizungumza na gazeti hili juzi, Wastara alikiri kuvunjika kwa ndoa yake huku akisema:
“Tangu nifunge ndoa sijawahi kuwa na furaha ndani ya ndoa hata mara moja kwani mume wangu alikuwa akinifanyia mambo siyo.
SIRI YA TATU
“Kabla hajanioa, aliniahidi vitu vingi ikiwemo kunifungulia maduka kwa
ajili ya kujiendeleza na vitu vingine vingi lakini hakuna hata kimoja
alichokifanya,” alisema Wastara.
SIRI YA NNE
Staa huyo
alikwenda mbele zaidi na kuanika siri ya nne akisema: “Nilipoona ndoa
imenichosha nikawa najaribu kutishia kuondoka, nikimwambia naondoka
alikuwa akiniambia njia nyeupe niondoke mapema ili mke wake (mkubwa) aje
kuishi. Inaonekana alitamani niondoke ili mke wake aje kukaa nyumbani.
Alisema mke wake hawezi kukaa hotelini na mimi nipo ndani.”
SIRI YA TANO
Ilidaiwa kuwa, siri nyingine iliyomfanya Wastara aachike ni kushindwa
kwake kukabiliana na uke wenza hasa ikielezwa kuwa, uvumilivu wa hali ya
juu unahitajika unapoingia kwenye ndoa ya sampuli hiyo.
“Unajua
siri nyingine ni kwamba, Wastara siyo mwanamke wa kuvumilia uke wenzake,
yapo baadhi ya mambo angevumilia lakini hakuwa mvumilivu, ikawa sababu
ya yeye kuondoka,” alisema rafiki wa karibu wa staa huyo.
AONDOKA NA MSICHANA WA KAZI
Wastara alisema kuwa, ameamua kuondoka kwa mwanaume huyo yeye na msichana wake wa kazi ‘hausigeli’ kwa kuwa alishachoka.
ANACHOJUA WASTARA
“Mimi najua watu wengi watasema na kuniona tofauti lakini kikubwa
naangalia furaha yangu iko sehemu gani, najuta sana kuingia kwenye ndoa
lakini nawashauri wanawake wenzangu kufikiria mara mbilimbili kabla
kuingia huko, kuna mambo mengi sana,” alisema Wastara.
HUYU HAPA MUME WA WASTARA
Sadifa Juma ndiye anayelalamikiwa na Wastara kwamba hakumtimizia yale
aliyomwambia lakini pia ndiye anayedaiwa kumpa talaka Wastara na si
kwamba, ameomba yeye.
Akijibu madai ya Wastara alipoongea na gazeti hili juzi kwa njia ya simu, alisema:
“Mimi si mgonjwa wa akili, Wastara ni mlemavu, hana baba wala mama
halafu leo hii nimseme vibaya. Mpaka nimeamua kumuoa ina maana
nilimpenda kwa nini nimfanyie vitu ambavyo sivyo?
“Lakini katika
hayo, pia mimi nimefundwa kwa kufundishwa kwamba mambo ya ndoa
hayapelekwi kwenye vyombo vya habari au Instagram. Na huyo aliyevianika
vitu vya mke wangu nitadili naye.”
MSISITIZO WAKE
“Ninachojua
mimi, Wastara bado ni mke wangu. Huyo mnayesema kwamba babu yake
ameongea kwenye redio akisema kwamba nimemwacha Wastara, talaka alitoa
yeye? Mambo ambayo mimi naweza kuyasema kwenye vyombo vya habari ni
kuhusu jimbo langu au mambo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni
chama changu.”
BOND: MIMI NIMESIKIASIKIA TU
Ijumaa lilimpigia
simu Bond juzi na kumuuliza kuhusu Wastara kuachika ambapo alisema: “Na
mimi nimesikiasikia na kusoma kwenye mitandao, hivi ni kweli?” (Ijumaa
likaachana naye bila kumpa jibu).
MAISHA YA UHUSIANO, NDOA YA WASTARA
Wastara amapitia katika maisha ya uhusiano na ndoa kwa wanaume kadhaa.
Mwaka 2000 alifunga ndoa na mwanaume anayeitwa Ahmed Kushi kutoka
Zanzibar na kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Fares.
Nyuma ya hapo, Wastara alizaa mtoto mmoja na Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.
Mwaka 2003, Wastara alifunga ndoa na msanii mwenzake wa filamu, Juma
Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye alifariki dunia mwaka, 2013. Walibahatika kuzaa
naye mtoto mmoja aitwaye Farheen.
Mwaka 2015, akafunga ndoa na
Mbunge Sadifa akitokea kwenye uhusiano na msanii wa filamu, Bond na
aliyodai kuyasema ndiyo hayo kwamba ameachika kwa talaka mbili huku
mumewe huyo akikanusha.
Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni,
habari zilitua Ijumaa kwamba Wastara ameugua ghafla baada ya sukari
kupanda akiwa mjini Morogoro na kulazwa Hospitali ya ST. Herry Health
0 comments:
Post a Comment