Mshambuliaji veterani wa Athletic Bilbao, Aritz
Aduriz, ameanza kwa kishindo mechi yake ya kwanza ya kimataifa kwa
kupachika bao na kuwapatia sare muhimu mabingwa watetezi wa Bara la
Ulaya timu ya Hispania.
Katika mchezo huo Italia ilikuwa ya kwanza
kupachika bao kupitia kwa winga wa timu ya Napoli Lorenzo Insigne
aliyepachika bao safi kufuatia mashambulizi ya kushitukiza.
Lakini Aduriz mwenye miaka 35, na ambaye amefunga
mabao 31 katika ligi ya La Liga akiwa na Athletic Bilbao,
alisawazisha bao hilo dakika mbili baadae na matokeo kuwa sare ya bao
1-1.
Aritz Aduriz akiteleza na kupachika bao la kusawazisha
Lorenzo Insigne akimpoteza kipa David De Gea na kupachika bao la kwanza
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment