MICHAEL JORDAN AONGOZA KUZICHANGA FEDHA KWA WACHEZAJI WALIOSTAAFU

Michael Jordan ambaye ndiye sura ya bidhaa za kampuni ya Nike ameendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa kulipwa fedha nyingi katika kundi la wanamichezo waliostaafu kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Mchezaji huyo mkongwe wa mpira wa kikapu, aliacha kucheza mwaka 2003 aliingiza dola milioni 110 mwaka 2015 na anakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni moja, kwa mujibu wa jarida hilo la biashara la Marekani.

Mauzo ya bidhaa za Nike Jordan yaliongezeka kwa asilimia 14 nchini Marekani katika mwaka jana, ambapo Jordan amempiku mchezaji soko nyota David Beckham wa Uingereza ambaye anashika nafasi ya pili.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment