Video
Queen nyota, Agnes Gerald maarufu kama Masogange anadaiwa kutaka
kumharibu muuza nyago chipukizi Asha Salum ‘Kidoa’ baada ya wadau
kutilia shaka ukaribu wao.
Kwa
mujibu wa chanzo cha uhakika, katika siku za hivi karibuni mabinti hao
wamekuwa na urafiki wa karibu, wakichati mambo mengi kwenye mtandao wa
kijamii wa Instagram, kitu kinachoonesha huenda ushosti wao ukafika
mbali zaidi ya hapo.
“Si
unajua Masogange ana zile dili zake za kwenda mara kwa mara Sauz huku
ikiwa haijulikani hasa anafuata nini? Na si unakumbuka ule msala wake wa
kukamatwa na madawa ya kulevya? Sasa wadau wanahofu asije naye
akaingizwa kwenye mchongo,” kilisema chanzo hicho.
Katika
kuweka sawa madai hayo, gazeti hili liliwasiliana na Kidoa ambaye
alifunguka; “Mimi ni mtu mzima na akili zangu timamu, siyo kila rafiki
utakayekuwa naye basi lazima uige tabia zake, halafu Masogange siyo
rafiki yangu kihivyo, kawaida tu!”
Kwa
upande wake, Masogange alipotafutwa na kuulizwa kuhusu madai hayo,
alijibu kwa kifupi; “Ulishawahi kuniona nikienda naye Sauz, au
ulishawahi kuniona naye kwenye ndege, kifupi mimi sinaga rafiki.”
0 comments:
Post a Comment