Kampuni
ya usafi ya Green WastePro Ltd iliyopewa zabuni ya kuhakikisha Manispaa
ya Ilala katika maeneo ya Mchafukoge, Kisutu, Kivukoni na Kariakoo
yanakuwa katika hali ya usafi imezindua magari mapya matano ya kisasa
ambayo yanataraji kurahisha ufanyaji kazi wa kusafisha na kukusanya taka
za maeneo ambayo wanafanya kazi.
Kampuni
hiyo imefanya uzinduzi wa magari matano ya kubebea taka ya kisasa na
lingine moja ambalo litakuwa linafagia barabara na hivyo kuwa na idadi
ya magari sita mapya.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kampuni ya usafi ya Green Waste
Pro Ltd, Anthony Mark alisema kuwa magari hayo niya kisasa na hawakuwahi
kuwa nayo awali hivyo kutokana na ujio wa magari hayo wanataraji kasi
ya kufanya kazi kuongezeka.
Alisema
kutokana na jinsi magari hayo yalivyotengenezwa wanaamini yatasaidia
kupunguza muda wa kufanya kazi kutokana na kuwa na uwezo wa kupakia
uchafu yenyewe na hivyo kupunguza muda tofauti na awali ambavyo walikuwa
wanatumia mikono katika magari yaliyokuwapo.
“Tunategemea
ufanisi zaidi sababu haya magari niya kisasa na yana beba hata uchafu
yenyewe kwahiyo kama kazi ilikuwa ya dakika 10 inaweza kufanywa kwa
dakika tatu,” alisema Mark.
Nae
mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Diwani wa Kata ya Mchafukoge, Mariam
Lulida aliwapongeza Green WastePro Ltd kwa magari ambayo wameongeza na
kuwataja kama moja ya kampuni ambayo wamekuwa wakifanya nao kazi kwa
kushirikiana kwa karibu.
Alisema
kuna baadhi ya changamoto bado zimekuwa zikijitokeza lakini wamekuwa
wakifanya mazungumzo ili kuona ni jinsi gani wanaweza kumaliza
changamoto hizo na kuendelea na kazi ya kuweka Manispaa ya Ilala katika
hali ya usafi.
“Ninawapongeza
sana kwa jambo hili na ninaamini tutazidi kufanya kazi kwa karibu nyie
ni wadau wetu na kama ni changamoto zinajitokeza ni ndogo ndogo na
tunazungumza na kuweka sawa.” alisema Bi. Lulida.
Aidha
diwani huyo alimpongeza Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuifanya
siku ya Jumamosi ya kila wiki kuwa siku ya usafi na tayari kumeanza
kuonekana mabadiliko kwa wananchi kujitambua na kutambua wana wajibu wa
kuhakikisha mazingira yanayowazunguka yanakuwa katika hali ya usafi.
Nae
Meneja Mwendeshaji wa kampuni ya usafi ya Green WastePro Ltd, Abdallah
Mbena alisema ununuzi wa magari hayo umegharimu kiasi cha Bilioni moja
na Milioni 600 na hivyo wanawaomba wananchi kushirikiana nao kwa kulipa
kodi ili wazidi kuendelea na kuboresha zaidi huduma.
Alisema
kwa sasa wamefikisha idadi ya magari 20 ambayo yanafanya kazi ya kubeba
taka na magari hayo mapya matano ya kubeba uchafu yana uwezo wa kubeba
Tani 12 kwa wakati mmoja na lingine moja linafanya kazi ya kufagia
barabara na hivyo kusaidia kupunguza ajali ambazo zilikuwa zinatokea
awali kwa wafanyakazi wa kampuni yao.
Meneja Mwendeshaji wa Green WastePro, Abdallah Mbene akitoa taarifa
kuhusu Kampuni ya Green WastePro wakati wa uzinduzi wa magari matano ya
kufanyia usafi.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi wa magari mapya Diwani wa kata ya Mchafukoge, Bi.
Mariam Lulida (nguo nyeusi) akielekea katika eneo la uzinduzi, Wa
kwanza kulia ni Afisa Mtendaji wa kata ya Mchafukoge, Luhungu Renatus,
Mwenyekiti wa Mchafukoge, Alhaji Masoud Mbilinyi, Mkurugenzi wa Green
WastePro, Anthony Mark.
Diwani
wa kata ya Mchafukoge, Bi. Mariam Lulida akikata utepe kuashirikia
uzinduzi wa magari mapya matano ya kubeba usafi ya Kampuni ya Green
Waste Pro. Kulia ni Mkurugenzi wa Green Waste Pro, Anthony Mark na
kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Green Waste Pro, Abdallah Mbene.
Diwani wa kata ya Mchafukoge, Bi. Mariam Lulida akiwa ndani ya moja ya magari ambayo yamezinduliwa na kampuni ya Gree WastePro
Diwani wa kata ya Mchafukoge, Bi. Mariam Lulida akiendesha mtambo wa kubeba taka na kuingiza ndani ya gari la kubeba uchafu.
Diwani
wa kata ya Mchafukoge, Bi. Mariam Lulida akisalimiana na baadhi ya
wafanyakazi wa Green WastePro mara baada ya kuzindua magari mapya matno
ya kufanyia usafi.
Wafanyakazi
wa Green WastePro wakishangilia uzinduzi wa magari ya kufanyia uasafi
yaliyozinduliwa na Diwani wa kata ya Mchafukoge, Bi. Mariam Lulida.
Wafanya kazi wa Green WastePro wakiwa katika picha ya pamoja.
Muonekano wa magari ambayo yamezinduliwa na kampuni ya Green WastePro
0 comments:
Post a Comment