China yajitahidi kutekeleza mtizamo wa usalama wa nyuklia



Katika miaka ya hivi karibuni, sekta ya nishati ya nyuklia ya China imeendelea kwa kasi, na idadi ya vituo vilivyopo na vinavyojengwa vya kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia vyote vinachukua nafasi ya mbele duniani. Wakati huohuo, China siku zote inafuata mtizamo wa kuhakikisha usalama wa nyuklia, na mfumo wa kukabiliana na hali ya dharura ya nyuklia umeendelea kukamilishwa.
Hivi karibuni, chombo cha kuhimili shinikizo kiliwekwa kwenye kinu cha nyuklia cha kwanza duniani chenye hali joto ya juu kinachopozwa kwa gesi aina ya HTGR katika kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha ghuba ya Shidao mkoani Shandong, hatua inayomaanisha kuwa China imepata maendeleo makubwa katika ujenzi wa kinu cha nyuklia aina ya HTGR na utengenezaji wa vifaa vya nyuklia. Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Yang Junhui amesema, mradi huo wa kielelezo ni kinu cha kwanza cha nyuklia duniani kinachotimiza vigezo vya usalama vya mfumo wa nyuklia wa kizazi cha nne.
"Kinu hiki kinaweza kujizima katika hali isiyo na nishati yoyote au bila umeme, umaalum wa kinu hiki aina ya HTGR tuseme ni nishati safi, hakitoi uchafuzi wowote, na pia kina ufanisi mkubwa na kinaweza kutumiwa kwa njia nyingi, umaalumu mkubwa ni kusanifiwa kwa kuzingatia vigezo madhubuti vya usalama."
Katika miaka ya hivi karibuni, teknolojia za China kwenye sekta ya nishati ya nyuklia zimeendelea kupiga hatua, na kwenye mchakato wa utafiti wa teknolojia mpya, usalama siku zote unapewa kipaumbele. Mhandisi mkuu wa kampuni ya miradi ya nishati ya nyuklia ya China Bw. Xing Ji amesema, kwenye usanifu wa teknolojia ya nishati ya nyuklia, usalama ni kitu cha kwanza kinachotakiwa kuzingatiwa.
Wakati wa kutafuta usalama kwa njia ya kuendeleza teknolojia, China pia imefanya uvumbuzi kwenye mtizamo wake juu ya usalama wa nyuklia. Mwezi Machi mwaka 2014, kwenye mkutano wa tatu wa kilele kuhusu usalama wa nyuklia, rais Xi Jinping wa China alifafanua kwa mara ya kwanza mtizamo wa China kuhusu usalama wa nyuklia kuwa ni kutilia maanani maendeleo na pia usalama, kutilia maanani haki na pia wajibu, kutilia maanani kujitegemea na pia ushirikiano, na kutilia maanani kutatua dalili za hatari na pia kuondoa mizizi yake. Mtizamo huo umetoa mwelekeo kwa China na hata dunia nzima katika matumizi ya nishati ya nyuklia kwa njia salama. Mkurugenzi wa idara ya nishati ya nyuklia katika idara kuu ya nishati ya China Bw. Liu Baohua amesema, ingawa asilimia ya umeme unaozalishwa kwa nishati ya nyuklia nchini China bado iko chini kuliko baadhi ya nchi zilizoendelea kwenye sekta ya nishati ya nyuklia, lakini kiwango cha usalama wa sekta hiyo ya China kinachukua nafasi ya mbele duniani.
"Vituo vya kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia nchini China havijawahi kukumbwa na ajali ya ngazi ya pili au zaidi, vigezo vyote vinachukua nafasi za mbele duniani; Ubora na usalama wa vinu vinavyojengwa vinaweza kudhibitiwa na vyote viko chini ya udhibiti. Baada ya kutokea kwa ajili ya nyuklia nchini Japan, tumechukua hatua madhubuti, kufanya ukaguzi kwa vituo vyote nchini China na kuvifanyia marekebisho muhimu. Baraza la serikali la China lilitoa mpango wa usalama wa sekta ya nishati ya nyuklia na mpango wa maendeleo ya sekta hiyo kwa muda mfupi na kipindi kirefu, utekelezaji wa mipango hiyo umeendelea vizuri, kazi muhimu za kufanya marekebisho ya kiusalama zimetekelezwa kwa utaratibu kama ilivyopangwa, na kiwango cha usalama kinaendelea kuimarishwa."
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment