March 29 2016 bodi ya shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4
kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni kufanyika kwa
uchaguzi Zanzibar licha ya malalamiko ya uchaguzi huo lakini pia sheria
mpya ya makosa ya mitandao Tanzania.
Sasa leo March 31 2016 shirika la utangazaji la Uingereza BBC kupitia bbcswahili.com limeandika ripoti ifuatayo >>> ‘kundi
la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi limetangaza kusitisha
ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania, hii inafuatia uamuzi wa
shirika la utoaji misaada la serikali ya Marekani kuondoa msaada
kutokana na uchaguzi wa Zanzibar ulivyoendeshwa‘
‘Karibu theluthi moja ya bajeti
ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za
hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya‘ – BBC SWAHILI.
0 comments:
Post a Comment