Mahakama Kuu ya Tororo nchini Uganda
imemuhukumu mwanaume mmoja miaka 29 jela baada ya kutiwa hatiani kwa
kumuua baba yake kikatili.
Mwanaume huyo Silver Oketch mkazi wa
Wikusi-Nyikisoza wilayani Tororo alihukumiwa adhabu hiyo na Jaji
Mkazi wa Mbale Henry Kaweesi baada ya kukiri kosa.
Mtuhumiwa huyo alikuwa akishtakiwa
kwa kosa la kumuua kwa kumkata kata kwa panga baba yake mzazi Sam
Oketch kwa madai ya kumuibia kuku wake.
0 comments:
Post a Comment