Watu 21 wafariki na wengine 66 wamelazwa baada ya wimbi la joto kuikumba Misri

Wizara ya afya ya Misri imesema takriban watu 21 wamekufa na wengine 66 kukimbizwa hospitali baada ya wimbi la joto kali kuyakumba maeneo yote ya nchi hiyo. Vifo hivyo vilivyotokea siku ya jumapili vimesababishwa na hali ya joto lililofikia nyuzi 47.

Wizara ya afya ya Misri imetoa tahadhari kwa wananchi hasa wenye umri mkubwa na wenye magonjwa sugu kama shinikizo la damu, kisukari na ugonjwa wa moyo kuchukua tahadhari na kutokaa kwenye maeneo yenye jua hususan mida ya jioni na kutotoka majumbani bila sababu ya msingi.

Msemaji wa mamlaka ya hali ya hewa ya Misri Bw Wahid Saudi amesema hali ya joto kali itaendelea hadi mwisho wa mwezi Agosti.

Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share



usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos 
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment