Tamasha la Kimataifa la utamaduni la Mombasa lilikamilika jana baada ya kudumu kwa muda wa siku kumi. Tamasha hilo lililovutia wageni kutoka sehemu mbalimbali lilianza tarehe 14 Agosti na kukamilika jana. Tamasha la utamaduni la Mombasa huandaliwa na serikali ya kaunti ya Mombasa ili kuvutia watalii na wawekezaji mjini humo.

Milio ya baruti na maonyesho ya fataki za kupendeza yaliipamba anga ya Mombasa eneo la Mama Ngina kuashiria mwisho wa tamasha la siku kumi la utamaduni la Mombasa.
Maelfu ya watu jana walijitokeza kusherehekea na kuhitimisha sherehe za tamasha la Mombasa lilioanza wiki iliyopita.
Tamasha hili huandaliwa kila mwaka na serikali ya kaunti ya Mombasa.

Kulikuwa na maonyesho mbalimbali ya utamaduni pamoja michezo aina tofauti,kutoka mashindano ya majahazi,uogeleaji,riadha,sanaa mbalimbali kama vile za uchoraji heena,uimbaji,densi na ngoma za kitamaduni.
Wageni kutoka sehemu mbalimbali za nchi ya Kenya na wale wa kutoka nchi za ng'ambo waliburudika mjini Mombasa kwa tamasha la siku kumi.
Tamasha hili lilivutia wageni na washiriki kutoka nchi za mbali kama vile kisiwa cha Mayotte nchini Ufaransa.


Jana wageni walifurahia mashindano ya kitamaduni ya majahazi na kutumbuizwa na kikundi kutoka kisiwa cha Mayotte ufaransa ambapo kikundi hicho kiliwaongoa waliohudhuria kwa nyimbo zao zenye mahadhi ya taarab.
Hali ya usalama mjini Mombasa imeimarishwa na kufikia jana vyombo vya usalama vimesema hakuna kisa chochote cha ukosefu wa usalama kilichoripotiwa wakati wa tamasha.
Mji wa Mombasa umekuwa na utulivu kwa muda wa mwaka sasa tangu kuripotiwe visa vya mashambulizi ya kufuatanishwa ya ugaidi.
Mwenyekiti wa chama cha utalii cha Mombasa na Pwani Bw Mohamed Hersi amesema kuwa tamasha hilo la kila mwaka litafufua matumaini ya kuvutia wageni katika pwani ya Kenya.
"Miezi sita ya kwanza haikuwa shwari kabisa hata tukawa tunajiuliza ni wapi Mombasa inaelekea.Mombasa inategemea sana utalii"
Gavana wa Mombasa Hassan Joho amesema kuwa kwa muda mrefu sasa kaunti ya Mombasa imeathirika na utangazaji hasi kutokana na matukio yasiyopendeza,jambo lililowapelekea kutafuta mbinu ya kuitangaza upya Mombasa kama kivutio cha utalii.
"Kwa muda sasa tumeathirika na matangazo hasi kutokana na visa vya mashambulizi ya kigaidi hivyo basi ikabidi tuje na njia mbadala ya kukabiliana na matangazo hasi"
Kwa mujibu wa katibu mtendaji wa serikali ya kaunti ya Mombasa anayehusika na utalii na utamaduni Bw Joab Tumbo ,tamasha hili limesaidia katika kuitangaza kaunti ya Mombasa na kuiweka katika ramani ya Kimataifa sio tu kama kivutio cha utalii kwa fukwe zake bali pia kama kivutio cha utalii kutokana na utamaduni.
"Tuko hapa kusherehekea utamaduni na tunasema kwamba wakati umefika wa kuiangalia Mombasa sio tu kama chaguo la utalii kwa fukwe za bahari bali pia kama chaguo la utalii kwa utamaduni na pia uwekezaji"

Tamasha hili limeandaliwa mwezi Agosti tofauti na mwaka jana ambapo liliandaliwa mwezi Desemba.
Tumbo anasema walifanya mabadiliko hayo kwa sababu Agosti ni mwezi wa likizo nchini Kenya.
"Tumefanya kusudi kusogeza tamasha hili hadi mwezi Agosti kwa sababu ni mwezi wa likizo nchini Kenya.Mwaka jana tulikuwa na tamasah la siku nne,kumekuwa na maendeleo makubwa"
Idadi ya watu iliendelea kuongezeka siku hadi siku tangu wiki iliyopita katika mji wa Mombasa huku biashara ikinoga kama wanavyoeleza baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la Mama Ngina.


Tamasha la Kimataifa la Mombasa kuhusu utamaduni lilianzishwa mwaka 2013 ambapo liliandaliwa kwa muda wa siku nne lakini hivi sasa,kuanzia mwaka huu,linaandaliwa kwa siku kumi.
Waandalizi wanasema tamasha limepata mafanikio makubwa sana kwa kuvutia watalii mjini Mombasa,huku kaulimbiu ikiwa ni "Tukutane Mombasa".
Zaidi ya watu 40,000 walihudhuria tamasha la Kimataifa la Mombasa,kuhusu utamaduni mwaka huu.
P yhaa tv coming soon

Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
 


face book ipyana stephen






  Share


















usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos 









Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment