kwa hali hii tutapona

fekiiii
Mmlaka ya chakula na Dawa TFDA imeatoa ripoti ya mwaka wa fedha kuhusu bidhaa mbalimbali zilizokamatwa na kuteketezwa kwa mujibu wa sheria na hatua zilizochukuliwa.
Mkurugenzi wa TFDA Hitti Sillo amesema  katika mwaka wa fedha wamekamata na kuteketeza vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku tani 16.61 ambazo thamani yake ni shilingi milioni 44.2.
‘Vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku vilivyoingizwa tumekamata vikiwa vinaingizwa nchini na vingine vimekutwa katika soko vikiwa tayari vimeingizwa na vingine vikiwa njiani  kuingizwa nchini, mara nyingine tumekamata mabasi yakiwa na vipodozi vinavyoingizwa nchini  kinyume cha sheria vyote hivyo thamani yake kwa mwaka wa fedha uliopita ni shilingi milioni 44″ Sillo.
Amesema kazi hiyo ni endelevu kwa kuwa TFDA ipo sehemu mbalimbali nchini na wakaguzi wake wapo kuanzia bandarini na katika viwanja vya ndege ambapo ndipo hukamataa bidhaa nyingi.
Amesema miaka mitatu iliyopita udhibiti umeimarika sana ndio maana matukio mengi ya kukamatwa kwa watu ambao wanaingiza vipodozi hatari kinyume cha sheria wanakamatwa wakiwa mipakani.

Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share

Tokeo la picha la twitter
comment
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment