Hali ya tahadhari imetangazwa katika
mji wa Marekani Ferguson. Mvutano ulienea baada ya kijana mweusi wa
miaka kumi na nane kujeruhiwa kwa risasi na polisi mwishoni mwa
maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Waendesha mashitaka
wametamka kuwepo kwa hatia kwa kijana Tyrone Harris ambaye yu mahututi
hospitalini.Kijana huyo alikua akishiriki katika maandamano ya
kuadhimisha mwaka mmoja tokea kifo cha rafiki yake Michael Brown, kijana
mweusi aliyeuawa na polisi mzungu mwaka wa jana ambaye baadaye
ilisemekana hakuwa na hatia.Polisi walisema Tyrone Harris alikuwa miongoni mwa watu sita ambao waliwafyatulia risasi maafisa. Baba yake anasema mwanaye hakua na silaha na alijaribu kukimbia kujihami.
0 comments:
Post a Comment