Wakati
mshambulizi Mrundi, Kelvin Ndayesenga akitaraji kurudi nchini
kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Simba SC, Betram Mwombeki ambaye
ni mshambulizi-pacha wa zamani wa Amissi Tambwe katika timu hiyo ya ‘
Mitaa ya Msimbazi’ katikati ya jiji la Dar es Salaam amefunguka na
kusema ni hadi pale viongozi/wahusika wa usajili katika timu hiyo
watakapoacha ‘ ubinafsi’ na kutengeneza mifumo mizuri ya kiutawala ndipo
wanaweza kupata mafanikio.
Akizungumza
na mwandishi wa www.shaffihdauda.co.tz ( Baraka Mbolembole) mapema
Jumamosi hii akiwa jijini Mwanza, Betram ambaye amepumzika kucheza mpira
wa ushindani baada ya kucheza nchi za Uganda, Rwanda, Kenya alisajiliwa
na Simba katikati ya mwaka 2013 akitokea nchini Marekani alidumu kwa
msimu mmoja tu katika timu hiyo licha ya kufanya vizuri sambamba na
Tambwe katika safu ya mashambulizi.
Hivi
navyoandika ni kwamba washambuliaji wote wawiwli, Betram na Tambwe
hawapo katika timu hiyo na klabu imekuwa ikitumia pesa nyingi kupata
wafungaji. Mwombeki amekosoa mfumo mzima wa kimpira, kiutawala huku
akisimulia baadhi ya matukio yasiyo vutia aliyowahi kukutana nayo ndani
ya klabu ya Simba.
Haya hapa mahojiano yangu na Betram……
www.shaffihdauda.co.tz; Umecheza Simba kwa muda mfupi lakini ulifanya vyema, nini sababu inayokufanya upumzike mpira kwa sasa?
Betram
Mwombeki; Sijapumzika kucheza mpira kila siku nacheza na nisipo cheza
basi nitafanya ‘matizi’ yoyote ya kuhusiana na shughuli hiyo , pia kwa
sasa nina shughuli zangu nyingine zinaendelea kama kawaida. Lingine siyo
kama niliachwa Simba ndiyo ‘ nakakasirika’ mpaka ifikie hatua ya
kuuchukia mpira au kuacha lakini mimi nachukia sana ‘system’ yetu ya
mpira wa kibongo kulinganisha na sehemu zingine nilipokuepo nacheza.
www.shaffihdauda.co.tz; Mfano, ni yapi hayapo sawa katika mfumo wetu wa mpira?
Betram
Mwombeki’; Mimi ni ‘mkubwa’ naongea kutoka moyoni na ukweli ‘ najua
watu hawapendi ukweli ukiongelewa’ na wanakuchukia lakini mie ‘ I don't
care’ kwani siku ya mwisho ukweli utatakiwa uongelewe ili tuweze
kujenga na kutatua ambacho kinasumbua
Naweza
nikasema kwamba mfumo wetu wa bongo umekuepo kama siasa ambayo ‘
imeingia uchafu ndani yake’ na ‘wadadu’ au wana ongoza soka letu la
bongo wengi wao siyo watu ‘ waliolifuzu’ kwenye hiki kitu au hawakuwahi
kucheza kuona ni nini wapaswa kufanya.
www.shaffihdauda.co.tz;
Ulipotoka Marekani na kujiunga Simba siku ya kwanza ulipofika mazoezini
uligundua tofauti gani kati ya maisha ya kimpira huko ulipokuwa na ile
ya Simba?
Betram
Mwombeki; Hahahahahaha siku ya kwanza sikuona kitu lakini tulivyo anza
kusafiri kwenda mikoani kucheza’ friendly games’ hapo kabla
hatujasajiliwa kuna kitu nilikiona nikasema hapa hamna kitu hii ni
‘miyeyusho mitupu’ , kwani timu ilikuwa inasafili kama timu ya ‘
ndondo’ bila camera man bila management yeyote bila jezi ya timu ili
tuweze ‘ kuadivatazi’ timu yetu yaaani vitu vingi sana kiasi kwamba
nikaona ni kitu cha kienyeji sana, tulivyo fika Tabora nilikataa kulala
kitanda kimoja na mchezaji mwenzangu yaaani noma na ‘ Rage akasema wewe
Mmarekani sana hapa Bongo’
Betram
Mwombeki; Hilo si kwenye timu tu, pia kwa hii ni system ya maisha ya
bongo tunakopi na kupesti ‘mimi nikiwa kocha wa timu hapa bongo
definitely ntaleta watu wangu na ntachukia watu wallio letwa na viongozi
wengine bila sababu hata kama kazi wanaweza’
Kwenye
Shirikisho la mpira la kibongo ni kama chama cha siasa yaani kama mimi
nikipata namleta na mdogo wangu na mdogo angu anamleta anaemfuata ili
tupige pesa sio kazi
www.shaffihdauda.co.tz;
Ulipewa fomu na kusaini baada ya siku ngapi tangu uliojiunga kwa
majaribio chini ya walimu, King na Julio?.
Betram
Mwombeki; Hahahaha kwanza walikuwa wanataka nisaini bure ‘ eti kwa
sababu walikuwa’ wananiona leo nakuja na Range kesho Benz aaah huyu
wakawa wanasema ‘ Mmarekani hataki pesa na hata haitaji pesa zenu
mtakazo mpa’ .
Wakaanza
kunipotezea muda kila wakati watu wangu walipokuwa wanaongea nao mpaka
nakumbuka kuna mechi moja tulikuwa tunaenda kucheza Tanga na Coastal
usiku wake watu wangu wakaja Bamba Beach kule camp na kuwaambia ‘ huyu
aendi Tanga mpaka kila kitu kiwe tayari hapa’.
Zilikuepo
zimebakia siku kadhaa tu kabla ya kufuingwa kwa usajili na nilikuwa
niende Azam lakini Azam walikuwa wamemaliza usajili na wanakwenda South
basi walivyo rudi wakasikia naenda Yanga hapo ndiyo Simba wakastuka na
kukamilisha mapema
www.shaffihdauda.co.tz; Nini kilitokea?
Betram
Mwombeki; Basi tu walikuwa wanataka nisaini bure lakini Namshukuru
Mwenyezi Mungu nilipata nilichokipata na lengo langu kubwa ni kucheza
nyumbani kwani nilikuwa nimecheza Uganda Rwanda na Kenya kidogo lakini
sikukamilisha malengo yangu sasa nikaona hapa itakuwa fresh , kwanza ni
home.
www.shaffihdauda.co.tz;
Ulifanya vizuri ulipocheza na Amis Tambwe miaka miwili iliyopita.
Kwanini wote hamko Simba SC kwa sababu?
Betram
Mwombeki; Kwanza naweza kusema timu zetu kubwa siyo za kujenga
wachezaji au kutengeneza wachezaji au kujua nani anafa kucheza na nani
kwani mwisho wa siku Kibadeni alikuwa hapewi mamlaka yote ya timu na
kufanya uamuzi wa mwisho kwa hilo labda mimi nilikuwa nafaa kucheza na
Tambwe au na mtu mwingine tofauti na Tambwe lakini they didn't c that na
pia Tambwe ni mchezaji ambaye anahitaji mtu wa ‘ kuchafua harafu yeye
anafagia’.
Nirudi
kwenye shwali lako tuliondoka wote kwa sababu ya system mbovu iliyokuwa
inaendeshwa pale na kulikuepo kuna uongozi mwingine nje ya ule wa
kikatiba, waliokuwa madarakani then walikuwepo wanaotaka kuingia
madarakani so wakachafua ili nao wapate yaaani ‘ usida juu ya usida’
www.shaffihdauda.co.tz;
Ungekuwa kiongozi wa Simba ungefanya nini ili klabu iwe na timu bora ya
muda mrefu?. Tunaizungumzia zaidi Simba kwa sababu ni klabu kubwa ya
michezo Tanzania pia umewahi kuajiriwa pale kama mchezaji.
Betram
Mwombeki; Duh kazi ngumu sana hiyo lakini cha kwanza nisingelikubali
timu iwe ya wanachama na kuruhusu matajili wawekeze kwenye timu hapo
tungepata uwezo wa kupata Academy ya muda mrefu ili tuweze kukuza vipaji
vya hapa kwanza kwani mimi sioni ‘ solution’ ya kukosa wachezaji hapa
na kwenda kuchukua sehemu nyingine .
Mwisho
kupitia pesa tutakazo zipata tuta invest kwene mambo mengine beside
mpira kama vile kujenga hotels kila mkoa kununua mabasi ya biashara
kujiingiza kwenye kilimo na ufugaji kujenga mashule na tunaanza hapa na
kuxpandi pole pole kwenda kimataifa pia na shughuli zote hizo ziitwe
Simba au ziusishe na jina hilo ili tupaishe timu yetu ijulikane duniani
kote..!!
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos
P yhaa tv coming soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos


0 comments:
Post a Comment