Wakati
Yanga wakienda kujificha Mbeya kwaajili ya maandalizi ya ligi kuu na
mechi ya ngao ya jamii, mabingwa wa Kombe la Afrika Mashariki “Kagame
Cup”, Azam FC wanaondoka leo asubuhi kuelekea Kisiwani Zanzibar kwa
ajili ya maandalizi zaidi.
Azam
FC inaingia msituni kujiwinda na mechi yao ya Ngao ya Jamii dhidi ya
Yanga itakayochezwa mwishoni mwezi huu kabla ya kuanza kwa mikikimikiki
ya Ligi Kuu Bara.
Kocha
mkuu wa kikosi hicho, Stewart Hall aliwapa mapumziko wachezaji wake
mara tu baada ya kuchukua ubingwa huo uliowafanya waandike historia mpya
kwani ni mara ya kwanza kutwaa Kombe hilo pia walicheza bila kuruhusu
bao hata moja langoni mwao.
0 comments:
Post a Comment