Nimekutana na stori kutoka Marekani New York ambako
wafungwa wawili waliohukumiwa kifungo cha maisha wametoroka jela siku
chache zilizopita huku wakiwaacha maaskari magereza kwenye mshangao
wakiwa hawaelewi ishu hiyo imetokeaje.
Stori kwenye headlines wakati huu jijini New York ni malalamiko kutokwa kwa wafungwa wa Clinton Correctional Facility
amabao wanawalalamikia maaskari hao kwa kuwatesa na kuwafanyia vitendo
vya kuhatarisha maisha yao kwa nia ya kutafuta ukweli kuhusu wafungwa
hao waliotoroka.
Wafungwa waliobaki walikuwa
wakichukuliwa mmoja mmoja na kupelekwa kwenye chumba maalum ambako
walikuwa wakipigwa, wakikabwa koo, wakibamizwa kwenye ukuta na vitendo
vingine vya mateso na maaskari hao na ikiwa wakishindwa kutoa taarifa
ambayo maaskari hao wanaitaka basi vipigo na mateso vinaongezeka.
Baadhi ya wafungwa wakaamua kupeleka mashitaka yako mbele ya Ofisa Mkuu wa Magereza, taarifa ikawafikia Serekali na sasa hivi maaskari hao wako chini ya uchunguzi.
Hapa chini nimekusogezea kipande cha video kinachoelezea jinsi hali ilivyo huko New York.
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

0 comments:
Post a Comment