Nyota
wa zamani wa Barcelona Xavi amemshawishi kocha wake wa zamani Pep
Guardiola siku moja kurudi klabuni hapo endapo atahisi ni muda muafaka.
Guardiola
alifurahia maisha yenye mafanikio akiwa na klabu hiyo yenye maskani
yake Camp Nou, kabla ya kuachana nao mwaka 2012, na kuelekea kunako
klabu ya Bayern ambapo mkataba wake utamalizika msimu ujao, huku kukiwa
na tetesi kuwa yuko mbioni kurejea Barcelona.
"Nilifurahia
kipindi kizuri na chenye mafanikio wakati nilipokuwa na Pep pale
Barcelona na naamini kwamba atafanya maamuzi sahihi siku moja ili kurudi
tena Barcelona", Xavi, ambaye kwa sasa yupo katika klabu ya Al Sadd,
alikaririwa na tovuti ya klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment