Mchezo wa soka kwa Afrika Mashariki umezidi kukua siku hadi siku pamoja na kukua soka la Tanzania bado linaongoza kwa kupokea wachezaji wa kigeni na kuwalipa vizuri, wachezaji kutoka Ligi za Kenya, Uganda na hata Rwanda huwa wanakiri kuwa Tanzania kuna ushabiki wa kweli wa soka pili Ligi ya Tanzania inalipa vizuri.
Licha ya sifa zote hizo Tanzania haijawahi kutoa mchezaji katika Ligi kubwa ila Kenya imewatoa wachezaji wawili kutoka familia ya moja McDonald Mariga Wanyama na Victor Mugubi Wanyama. Wakenya hawa wameweka rekodi Afrika Mashariki ambayo kuivunja sio kazi ndogo.
Mariga ni kaka wa Victor mwaka 2010 aliweka rekodi ya kuwa Mwafrika Mashariki wa kwanza kutwaa taji la UEFA lakini mwaka 2013 mdogo wake Victor Wanyama
akaingia katika headlines ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika
Mashariki kucheza Ligi Kuu Uingereza lakini pia akaweka rekodi ya kuwa
mchezaji aliyeuzwa kwa gharama ya juu pound millioni 12.5 kutoka Celtic kwenda Southampton.
0 comments:
Post a Comment