KUHUSU UJIO WA FALCAO CHELSEA, HII NDIO KAULI YA COSTA.
Diego
Costa amesema kuwa ameshukuru sana baada ya kuona Radamel Falcao hakuwa
na msimu mzuri katika klabu ya Manchester United hali iliyopelekea
Chelsea kumnasa kirahisi.
Mkolombia
huyo amesajiliwa na Chelsea kwa mkopo wa msimu mzima akitokea Monaco
baada ya msimu uliopita kuitumikia Man United kwa mkopo pia.
Mourinho
alifichua kuwa mshambulizi huyo aliamua kupunguza mshahara wake ili
kuwaonesha mashabiki wa mpira Uingereza kuwa bado yuko vizuri.
"Ni
nzuri sana kwetu kwamba Falcao hakuwa na msimu mzuri wakati akikipiga
United na ndio maana kwa sasa tuko naye",alikaririwa na Daily Mail.
"Sote
tunafahamu kuwa Falcao ana kipaji kikubwa sana. Kitu pekee anachohitaji
ni kuaminiwa na kupendwa, na vyote hivyo atavipata hapa.

0 comments:
Post a Comment