
Kwa
matokeo hayo Simba wamejiwekea kibindoni alama 44 huku wakiwa wamecheza
michezo 25 na Azam wana alama 45 wakiwa wamecheza michezo 24.
Vita
hii inaonekana kuwa ngumu sana baina ya timu hizi mbili huku kila timu
ikionekana kuitolea macho nafasi ya pili baada ya Yanga kutangazwa
mabingwa wapya msimu huu mara baada ya kujikusanjia pointi 55 katika
michezo 24 waliyocheza ambapo si Azam wala Simba watakaoweza kuzifikia.
Azam
watajilaumu kwa kupoteza mchezo wa leo kutokana na kiungo wake mahiri
Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutolewa nje kwa kadi nyekundu mara baada ya
kumchezea madhambi beki wa kushoto wa Simba Mohammed Hussein
‘Tshabalala’ katika dakika ya 38.
Simba
walijipatia mabao yao kupitia kwa Ibrahim Hajib dakika ya 48 mara baada
ya kupokea krosi maridhawa kutoka kwa kiungo mahiri wa timu hiyo kinda
Said Ndemla , huku Ramadhan Singano 'Messi' akishindilia Msumari wa
mwisho golini kwa Azam mnamo dakika ya 75 baada ya kuachia shuti kali
lililomshinda mlinda mlango wa Azam, wakati wana lamba lamba Azam
walijipatia goli lao kupitia kwa kiungo wao Mudathir Yahya mnamo dakika
ya 57 kutokana na pasi nzuri aliyoipata kutoka kwa Kipre Tchetche.
Kwa
matokeo haya, Simba wanatakiwa kushinda mchezo wao wa mwisho huku
wakiiombea Azam ipoteze michezo yake miwili iliyosalia, ambapo itacheza
na Yanga na baadaye kumalizia na wanajeshi wa Mgambo JKT kutoka
mkoani Tanga
Simba
SC ; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joseph
Owino, Juuko Murusheed, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’/William
Lucian ‘Gallas’ dk85, Said Ndemla/Elias Maguri dk75, Ibrahim Hajib,
Emmanuel Okwi na Awadh Juma.
0 comments:
Post a Comment