Na Kassim Mtolea
Uwanja
wa Nangwanda sijaona mkoani Mtwara leo unatoa hukumu kwa timu ya
Ndanda fc kama itabaki ama itashuka kwenye mashindano ya ligi kuu msimu
huu.
Timu
hiyo ngeni kwenye ligi kuu inatupa karata yake ya ishirini na tano
mbele ya "wanankurukumbi"timu ya Kagera sukari kutoka kule mkoani
Kagera.
Akizungumza
na MPENJA BLOG katibu mkuu msaidizi wa timu hiyo Seleman Kachele
amesema kwa upande wao wapo kamili kupamba na wakata miwa hao.
"Tunajua
Kagera ni wazuri na ni wakongwe katika ligi lakini tutahakikisha
tunafanya kila liwezekanalo kuondoka na ushindi hii leo hapa nyumbani na
kufufua matumaini ya kubaki ligi kuu kwa msimu ujao naamini tutapata
ushindi hii leo dhidi ya wapinzani wetu hao".
Pia
katibu huyo amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuwa na utulivu kipindi
hiki ligi inapoelekea ukingoni na kuwataka wapenzi na mashabiki pamoja
na wanachama kuungana na kuwa kitu kimoja kuinusuru timu yao.
"Mwenendo
wetu hauridhishi hata kidogo lakin hatupaswi kukata tamaa niwaombe
mashabiki wapenzi na wanachama kuunganisha nguvu kwa pamoja ili
kuisaidia timu yetu imalize salama michezo yake miwili iliyobaki ikiwa
ni mchezo wa leo na ujao dhidi ya Yanga".Alisema Kachele.
Lakini
wakati Ndanda wao wakisema hivyo kwa upande wao wakata miwa Kagera
Sukari tayari wameshaingia mkoani humo na wapo tayari kwa kulipa kisasi
mbele ya wamakonde hao.Kocha msaidizi wa timu hiyo Mrage kabange amesema
wala hatishwi na tambo za wenyeji wao hao.
"Waache
waongee ni haki yao maana wapo nyumbani kwao pia ni uwanja wao kwahiyo
wanayo sababu ya kuzungumza lakini sisi kilichotuleta huku ni alama tatu
na wala sio maneno tupo tayari kwa mchezo na watu watajua
kitakachotokea hapo hapo baadaye we nitafute baada ya mechi nikupe
matokeo".Alihitimisha Kabange.
Huo
utakuwa ni mchezo wa pili kwa timu hizo kupamba katika ligi kuu ambapo
katika mchezo wa awali uliipigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza kama
uwanja wa nyumbani timu ya Kagera Sukari ilikubali kichapo cha goli
mbili kwa moja na kupelekea timu hiyo kukimbilia mkoani Shinyanga kwwnye
uwanja wa Kambarage huku kambi ya timu ikibaki jijini Mwanza
0 comments:
Post a Comment