Kuhusu ishu ya Shilole na BASATA, Snura kayatamka haya ..!!

SNURAAAA 
Wiki iliyopita kulikuwa na vichwa vya habari kuhusu Baraza la Sanaa Taifa kutoa barua ya Onyo kwa msanii Shilole baada ya kuonekana akiwa wazi sehemu za juu ya mwili wake jukwaani kwa bahati mbaya kwenye show yake  aliyoenda kuifanya Ubelgiji.
Shilole na Snura ni watu ambao wanafananishwa na kupambanishwa na wakati mwingine kulinganishwa kwenye muziki wanaoufanya..
Snura ameanza hivi>>’Kiukweli kabla sijataka kusema itakuaje, mimi binafsi kutoka kwenye moyo wangu namuombea sana msamaha na Watanzania wasimuangalie hivyo ambavyo wanamuangalia
Sentensi nyingine Snura amesema>>’Ile ni kama ajali hivyo wamuelewe kama ambavyo mwenyewe amesema yule ni mtu mzima na ana maumivu yake ndani ya moyo kwa hiyo unapozidi kumkandamiza ni kama unazidi kumuumiza kikubwa ni kumsamehe na kuona  je itatokea tena?
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment