Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford akipozi kimahaba na Rammy Galis.
Huenda maumivu
ya mapenzi yakazidi kumuandama msanii wa muziki Bongo, Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya gazeti hili kunasa picha za
mchumba’ke Shamsa Ford akiwa katika mahaba mazito na msanii mwanaume
mwingine aliyedaiwa kuwa ni mchepuko wake, Rammy Galis, Amani
lilifuatilia hatua kwa hatua.
Ishu hiyo ‘ilidakwa’ na ‘balozi’ wa gazeti hili usiku wa Jumapili
iliyopita ndani ya Ukumbi wa New Maisha, Masaki jijini Dar kulipokuwa na
onesho la Mrs. Mabeste Charity hafla iliyokusanya mastaa kibao na
watoto wengi wa mjini.
Katika pitapita zake huku akikodoa macho kila kona ndani ya ukumbi huo,
mwandishi wetu alibahatika kuwaona wawili hao wakiwa wamegandana kwa
staili ambayo si ya kujadili katiba mpya huku ukaribu na kutazamana kwao
kukiwa na maswali mengi kuliko majibu.
...Wakisakata rumba.
Hata hivyo, umbali wa mkao wao ulianza kupungua kila dakika moja
ilipopita wakawa wanabadili mapozi yakiwemo kutazamana kimahaba na
kushikana kwa kujitawala.
Baada ya kuhakikisha kuwa amepata picha za ushahidi wa kutosha,
mwandishi wetu aliwafuata wawili hao na kumuuliza Shamsa kama huyo ndiye
mbadala wa Nay, akamwambia mwandishi kuwa haikuwa kazi yake kujua kwani
pale walikuwa eneo la starehe hivyo hawakutaka bughudha na karaha
yoyote.
Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford.
“Ebwana ee, mbona hivyo jamani? Siyo kazi yako kujua huyu ni nani
kwangu, ni msanii mwenzangu na hapa tuko kwenye sherehe na hatuhitaji
usumbufu wowote,” alisema kwa mkato Shamsa.
Kwa upande wake Galis, alisema hana cha kusema kwani hakuwa eneo la mahojiano.
“Kaka huyu ni msanii mwenzangu na hapa si sehemu ya mahojiano,” alijibu.
0 comments:
Post a Comment