Aunty Ezekiel afunguka sababu ya kutomualika Wema kwenye sherehe yake
Uhusiano wa mastaa wawili wa Bongo Movie,Wema Sepetu na Aunty Ezekiel
wadaiwa kuwa tete sababu kubwa ikielezwa kuwa Aunty kupost kwenye
akaunti yake ya Instagram tangazo la shoo ya Zari White Party
iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu Mlimani City,jijini Dar.
Sababu nyingine inayofanya mashabiki kuamini mastaa hao kuwa wamegombana
ni hivi karibuni Aunty Ezekiel kufanya sherehe ya Baby Shower
iliyofanyika kwenye Bustani za Ndoto Polepole zilizopo Bagamoyo,Pwani
kumualika hasimu wa Wema,Kajala,ambapo Wema hakuwepo.
Katika sherehe hiyo Wema hakuwepo,hata hivyo Aunty Ezekiel
akizungumza na Uheard ya Soudy Brown,alisema kuwa hana ugomvi na Wema na
sababu ya kutomualika kwenye sherehe yake ni kuwa msanii huyo alikuwa
anashuti filamu.‘Sijagombana na Wema,sikumualika kwenye baby shower kwa sababu alikuwa bize anashuti video,’alisema Aunty.
0 comments:
Post a Comment