MKATABA, HATI NA MAMBO 11 YA MUUNGANO
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius
Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar.
Ulithibitishwa na Bunge la
Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi
hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana
hati za Muungano.
Sheria za Muungano ilitamka kwamba,
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika, kuwa
dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina
ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964.
Msingi wa katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati
za Muungano za Mwaka 1964.
Hati za Muungano zilitiwa saini
na Nyerere na Karume, Aprili 22, 1964 na hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola
moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere
alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Aprili 26, 1964, bunge la
Tanganyika lilipitisha sheria za Muungano, ambazo baadayezilithibitishwa na
Baraza la Mapinduzi Zanzibar.
Mnamo Aprili 27, 1964 waasisi
wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba wa Baraza la
Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika
na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu,
Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil.
Kati yao,
Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai.
Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianisha mambo 11 ambayo yalikubalika kuwa ni
ya Muungano ambayo ni; Katiba na Serikali ya Muungano, Mambo ya nchi za nje,
Ulinzi, Polisi, Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, Uraia,
Uhamiaji, Mikopo na Biashara za nje, Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa
forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa Tanzania unaosimamiwa na idara ya
forodha, Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
Katiba ya muda ya mwaka 1965
ilianisha utawala wa serikali ya mfumo wa chama kimoja, TANU kwa Bara na ASP
kwa Zanzibar. Katiba hii, ilizingatia misingi ya makubaliano ya Muungano ya
mwaka 1964 na sheria za Muungano wa Tangayika za Zanzibar.
Katiba hiyo ilianisha serikali
mbili, uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Muungano ikiwa na mamlaka juu ya
mambo yote ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa
Tanganyika. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa na mamlaka juu ya mambo
yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.
Hata hivyo mambo ya
Muungano yaliongezwa kutoka 11 hadi 22 kutokana na mahitaji ya ndani ya nchi
pamoja na mabadiliko yaliyokuwa yanaendelea kutokea ulimwengini baada ya
Muungano.
Mwaka 1985, jambo la 12
linalohusu sarafu na fedha kwa ajili ya malipo na kurahisisha usimamizi wa
fedha za kigeni na benki katika Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania, liliingizwa.
Kufuatia kuundwa kwa Jumuiya ya
Afrika Mashariki mwaka 1967, mambo matatu ya Muungano yaliyongezwa, ambayo ni
leseni za viwanda na takwimu; elimu ya juu; na usafirishaji wa anga.
Mwaka 1968, mambo ya maliasili
ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya magari na ama ya petroli na aina
nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia yaliyongezwa kwenye orodha hiyo.
Aidha mambo ya Muungano yaliendelea kuongezeka hadi
kufikia 21 kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwaka 1992 kufuatia mabadiliko
ya mfumo wa siasa nchini suala la 22 la uandikishaji wa vyama vya siasa na
mambo mengine yanayohusiana navyo liliongezwa kwenye orodha hiyo.
MJADALA KUHUSU MUUNGANO
Katika miaka hivi karibuni kumekuwa na mijadala
mbalimbali kuhusiana na muundo wa Muungano, baadhi wakitaka uwe wa zaidi ya
serikali mbili, wengine serikali moja, wapo wanaotaka Tanganyika iwe kivyake na
Zanzibar kivyake.
Hata hivyo hekima inaonyesha
kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unabaki kuwa ni fahari ya Watanzania,
kwani mwelekeo wa dunia katika nyanja mbalimbali, mataifa kuungana kwa
ushirikiano wa aina mbalimbali ni muhimu kuliko taifa moja kupambana kivyake.
Urejeaji wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki baada ya kuvunjika mwaka 1977, uwepo wa SADC, ECOWAS, COMESA, na
jumuiya nyingine nyingi duniani kote, ni vielelezo kwamba ushirikiano baina ya
mataifa ni suala lisilohitaji mjadala.
Ieleweke kwamba hakuna
ushirikiano usio kuwa na matatizo kama ilivyo kwa Muungano wa Tanzania, vivyo
hivyo muungano mwingine kama vile ya United Kingdom (UK), Uingereza na United States
of America (USA) kwa maana ya Marekani na United Arabs Emirate (UAE), nayo ina
matatizo, lakini hata mara moja mjadala juu ya matatizo hayo siyo kuvunja
ushirikiano bali kutatua na wale wanaotaka kuvunja hushughulikiwa ipasavyo.
"Matatizo ya Muungano kama
wa UK ni mabaya zaidi, na hata UAE hawana ahueni, ila wanajua kwamba Muungano
wao ni lazima. Wamarekani wanapambana na watu wenye mawazo haya ya kuvunja
miungano kwenye majimbo ya Alaska, Hawaii na Texas na mwishowe wameamua kuweka
kambi kubwa ya jeshi la nchi kavu Texas; utitiri wa kambi za anga Alaska; na
vituo vikubwa kupindukia vya majini kule Hawaii. Hivi, hawa mabingwa wa
demokrasia wanapoamua kulinda nchi yao namna hii, unafikiri ni wajinga?
Walimwaga damu na waliyanunua majimbo haya na wamepitia shida kubwa, ndiyo
maana leo wanajidai," anaandika mchangiaji katika mjadala kuhusu Muungano.
Ni vyema Watanzania
wakati huu wa kusheherekea miaka 51 ya Muungano, kila mmoja akajisikia ufahari
wa kuwa na kitu kizuri kilichoasisiwa na Waafrika wenyewe na kudumu kwa umri
huo.
Mawazo ya
kubaguana kwa sababu zisizo na msingi, pengine kukidhi matakwa na wakati kama
vile ya kibinafsi na kisiasa, yasipewe nafasi kuisambaratisha nchi. Chambilecho
wahenga, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
hata
hivyo mvutano huu umezidi kuigawa nchi hii kwa kuwepo kwa upinzani
miongoni mwa vyama vya siasa hasa vile vinavounda Umoja wa katiba ya
wanancho {UKAWA} dhidi ya Chama tawala {CCM}
Tundu Lisu, mwanasheria wa Chadema na mbunge wa Iramba Mashariki |
mmoja kati ya wanasiasa ambao walibadilisha hali ya
hewa bungeni miaka ya hivi karibuni kutokana na matamshi ya kuukashfu muungano
na waasisi wake ni tundu lisu, mwanasheria wa chadema na mbunge wa iramba
mashariki ambaye aliwafananisha waasisi hao na wahuni.
Je! Ni haki kwa mtu kama nyerere au karume kuingizwa
katika siasa ya sasa na kujadiliwa kwa kejeli?
Tunaelekea kusherehekea muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ni muda wako sasa kutafakari ikiwa muungano una tija au ni shida kwa
taifa lako, kwangu mimi hauharibu kitu maana Zanzibar na bara ni ndugu si wa
muungano tu bali ni wa damu.
0 comments:
Post a Comment