Najua kama ni mtumiaji wa usafiri
wa ndege utakuwa ushasikia taratibu za abiria kuzima simu wakati ndege
inataka kupaa na kutua ila huenda hukawa hujui sababu kwa nini unatakiwa
kufanya hivyo, inawezekana ulishajiuliza usipozima unaweza kusababisha
ndege kupata ajali au? jibu ni Hapana, isipokuwa unaweza kusababisha muingiliano wa mawasiliano kati ya rubani na waongozaji.
Vibrations au miungurumo ya simu na
vifaa vingine vya electronics vinahusika kwa kiasi kikubwa kuvuruga
mawasiliano mazuri kati ya rubani na wanaomuongoza, hivyo huwa
tunashauriwa kuzima simu na vifaa vingine vya electronics wakati wa
kupaa na kutua kwa ndege. Hiyo ni moja kati ya sababu kuu zilizotajwa
juu ya swali la ”Kwanini tuzime simu wakati ndege inaporuka na kutua”?.
0 comments:
Post a Comment