Cristiano Ronaldo amemuunga mkono kocha ajaye wa Manchester United, Jose Mourinho, kurejesha siku nzuri za kufanya vyema kwa klabu hiyo wakati huu Mreno huyo akitarajiwa kutangazwa hii leo.
Mashetani hao Wekundu na Mourinho wamekuwa katika majadiliano baada ya kumfukuza kocha Louis van Gaal na kwa sasa anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa Manchester United.
Ronaldo, aliyeichezea Manchester United kwa miaka sita, anamatarajio Mourinho ataibeba klabu hiyo na kuirejesha katika kiwango cha juu cha ubora duniani.
Sir Alex Ferguson akiwa na Cristiano Ronaldo


0 comments:
Post a Comment