Arsene
Wenger ametetea sera yake ya usajili, licha ya Arsenal kushindwa
kununua mchezaji yeyote wa ndani ya uwanja mpaka kufungwa kwa dirisha la
usajili wa majira ya kiangazi juzi.
Golikipa, Petr Cech ndiye mchezaji pekee aliyesajiliwa kwa paundi milioni 10 kutokea Chelsea.
Ukweli unaonesha kuwa Arsenal ya Wenger ndio klabu kubwa katika ligi tano za Ulaya ((Premier, La Liga, Serie A, Bundesliga na Ligue 1) ambayo haijanunua mchezaji wa ndani.
Hata mabingwa wa Hispania, Barcelona ambao kwasasa wamefungiwa usajili, waliweza kununua wachezaji wawili wakubwa.
Walimsajili kiungo wa Uturuki, Arda
Turan kutokea Atletico Madrid kwa paundi milioni 25 na kiungo wa
Sevilla, Aleix Vidal kwa ada ya paundi milioni 12.5, ingawa wote
hawatacheza mpaka 2016.
Kitendo cha Gunners kutosajili, kimewaudhi mashabiki waliokubuhu wa timu hiyo 'Arsenal Supporters Trust' ambao wamehitaji sera ya usajili ya Wenger ichunguzwe haraka.
Lakini
Wenger ambaye jana usiku alikuwa Nyon, Uswisi kwenye mkutano wa 2015
wa makocha wa juu wa UEFA ambapo alikutana na mpinzani wake wa zamani
Sir Alex Ferguson alisema:
"Nina furaha na uwekezaji nilioweka? ndiyo, kila muda.
"Mwaka uliopita, nilimnunua (Alexis) Sanchez, nilimnunua (Mesut) Ozil, nilimnunua Cech, nilimnunua Gabriel".
P yhaa tv coming soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos


0 comments:
Post a Comment