Anthony Martial mchezaji mpya wa Manchester United
Klabu
nchini Uingereza, vilivunja rekodi ya kutumia pesa nyingi zaidi katika
historia ya Ligi ya Premier majira ya joto huku pesa zilizotumiwa na
vilabu hivyo katika mwaka mmoja zikifika £1bn kwa mara ya kwanza.
Katika
kipindi cha kuhama wachezaji kilichomalizika siku ya Jumanne, vilabu
vilitumia £870m, 4% juu ya rekodi iliyowekwa mwaka uliopita.
Ukiongeza £130m zilizotumiwa na vilabu hivyo dirisha fupi Januari, kiasi hicho kinafikia £1bn.
Kilabu
ya Manchester City ilitumia pesa nyingi zaidi, ikinunua wachezaji
wawili bei ghali zaidi, £55m kwa Kevin De Bruyne kutoka Wolfsburg na
£49m kwa Raheem Sterling kutoka Liverpool.
Usajili
wa Manchester United wa £36m kumchukua mchezaji wa Monaco, Anthony
Martial, ulikuwa wa juu zaidi siku ya mwisho ya kuhama wachezaji.
Gharama yake inaweza kupanda hadi £58m ukiongeza vikolezo vingine.
Tangu
kuanzishwa kwa mfumo wa kuwepo kwa awamu ya kuhama wachezaji 2002,
jumla ya pesa zilizotumiwa imezidi £7.3bn, zaidi ya 80% ya kiasi hicho
zikitumiwa majira ya joto, kwa mujibu wa wadadisi wa kifedha wa
Deloitte.
Kuhamia kwa Kevin De Bruyne, Manchester City, ndiko kulikokuwa ghali zaidi sokoni.
Manchester
City walivunja rekodi ya klabu hiyo mara mbili awamu iliyopita ya
usajili kwa kuwanunua De Bruyne na Sterling na kuwafanya kuwa klabu
iliyotumia pesa nyingi zaidi kwa awamu moja nchini Uingereza.
Jumla
ya pesa walizotumia ya takriban £160m, inazidi takriban £150m
walizotumia Manchester United, majira ya joto 2014, wachezaji wengine
waliowanunua wakiwa Fabian Delph, Patrick Roberts na Nicolas Otamendi.
Viongozi
hao wa sasa wa Ligi ya Premia walipata afueni majira ya sasa ya joto
baada ya kuondolewa vikwazo vya matumizi ya pesa walipotimiza lengo
walilowekewa chini ya sheria mpya ya haki na usawa.
City
walikuwa wamewekewa kiwango cha juu cha matumizi cha £49 mwaka 2014 na
walitozwa pia faini ya £16.3m kwa kukiuka kanuni za Uefa.
Vilabu
vinne vya Ligi ya Premier, vinavyoshiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
msimu huu Manchester City, Manchester United, Chelsea na Arsenal
vilitumia kwa jumla takriban £340m, ikiwa ni karibu 40% ya jumla ya pesa
zilizotumiwa na klabu za Ligi ya Premier, kununua wachezaji.
Kununuliwa
kwa Martial mwenye umri wa miaka 19, Everton kumnunua mlinzi wa
Argentina Ramiro Funes Mori, kwa £9.5m na Papy Djilobodji kununuliwa £4m
na Chelsea kutoka Nantes, siku ya Jumanne kuliwezesha awamu hii ya
usajili kupita £835m zilizotumiwa mwaka jana.
Liverpool
wametumia pesa zaidi kuwasajili wachezaji saba, Christian Benteke
(£32.5m), Roberto Firmino (£29m) na Nathaniel Clyne (£12m) wakiwa ndio
ghali zaidi.
Manchester
United pia wamekuwa mbioni, wakitumia £139m kununua Martial, Memphis
Depay, Matteo Darmian, Bastian Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin,
huku Chelsea wakisubiri hadi dakika za mwisho kununua wachezaji wa
thamani, wakiwachukua Pedro, Baba Rahman na Djilobodji.
Kilabu iliyopandishwa daraja majuzi ya Watford ndiyo iliyonunua wachezaji wengi zaidi ligini, ikiwapata wachezaji 15 wapya.
P yhaa tv coming soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos


0 comments:
Post a Comment