KATIBU MKUU WA CHADEMA DK. WILLIBROD SLAA SASA AJITOA RASMI CHAMA CHA CHADEMA

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema) Dk. Willibrod Slaa amevunja ukimya hii leo kuhusiana na chama hicho kwa kuwashutumu viongozi wa chama hicho kwa kuwakumbatia wagombea waliokimbia CCM ambao amewaita kuwa ni makapi.

Katika mkutano huo alioufanya leo Jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa amesema yeye alitangaza hadharani kuwa Chadema haitopokea tena wagombea makapi, lakini viongozi wenzake wakaamua kumeza maneno yao na kuamua kuchukua makapi.

Akizungumzia suala la yeye kujiuzulu wadhifa ndani ya Chadema Dk. Slaa amesema aliandika barua mara mbili za kujiuzulu ambapo moja wapo alimuandikia Makamu Mwenyekiti wa Chadema Prof. Abdalah Safari, na kwa sasa yeye hana chama chochote cha siasa.

Aidha, Dk. Slaa ametumia mkutano huo kukanusha tuhuma kuwa mkewe Josephine Mushumbushi amepokea fedha ili amshawishi yeye kukisaliti Chadema na kumkataa Mh. Edward Lowassa.
P yhaa tv coming soon

Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
 


face book ipyana stephen






  Share


















usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos 





Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment