Chelsea
wameonywa kwamba wanaweza kulipa dau linalokaribia kufikia rekodi ya
dunia kama wanataka kumsajili kiungo wa Juventus, Paul Pogba, wakati wa
dirisha dogo la mwezi Januari mwakani.
Majira
ya kiangazi mwaka huu, nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ilikuwa
katika rada za Jose Mourinho ambaye aliweka mezani ofa ya paundi milioni
54, lakini .
Juventus waligoma kabisa kumuachia kijana huyo mwenye miaka 22.
Hatimaye, mkurugenzi mkuu wa Juventus, Giuseppe
Marotta ameonya kuwa Pogba ambaye ameimarika kuwa moja ya viungo mahiri
duniani ana thamani ya Euro milioni 100 sawa na paundi milioni 73.
Dau
la paundi milioni 86 walilolipa Real Madrid katika usajili wa Gareth
Bale kutokea Tottenham ya England, ndilo linashikilia rekodi ya dunia
na Marotta anaamini dili la Pogba litakaribia mzigo huo.
"Kwa
vile tunataka kushinda, tumeamua kuwabakiza wachezaji muhimu kama
Pogba, ingawa tulikuwa na ofa nyingi kutoka klabu muhimu". Marotta
amewaambia waandishi wa habari jana.
"Hapo baadaye atakuwa na thamani ya Euro milioni 100 (Pogba)".
Mfaransa
huyo ambaye amejaaliwa kasi, nguvu na ufundi alijunga na Juventus mwaka
2012 kutokea Manchester United na ameisaidia timu yake kurudisha makali
katika soka la Italia.
Juventus,
mabingwa wa Serie A katika miaka minne iliyopita, wameanza msimu huu
kwa kupoteza mechi mbili za kwanza na Marotta amekiri kwamba ni vigumu
kupata warithi wa Andrea Pirlo, Arturo Vidal na Carlos Tevez, ambao wameondoka majira ya kiangazi.
Kwasasa
Pogba yuko Ufaransa ambapo anatimiza majukumu ya timu ya Taifa ya nchi
hiyo inayojiandaa na fainali za EURO 2016 zitakazofanyika nchini humo.
0 comments:
Post a Comment