China yakumbuka ushindi dhidi ya Japan

Maadhimisho ya miaka 70 ya ushindi wa vita dhidi ya uvamizi wa Japan na vita dhidi ya ufashisti duniani yameanza leo saa 4 asubuhi mjini Beijing. Rais Xi Jinping wa China amehutubia maadhimisho hayo na kutoa wito kwa dunia nzima kukumbuka historia na kuthamini amani.
Rais Xi amesema katika vita dhidi ya uvamizi wa Japan, watu wa China walitoa mchango mkubwa kwa ushindi wa vita dhidi ya ufashisti duniani kwa kujitoa mhanga kwa wingi, na ksema njia nzuri zaidi ya kuadhimisha ushindi huo ni kuzuia vita kama hiyo isitokee tena. Amesisitiza kuwa lengo la kuadhimisha ushindi huo ni kukumbuka historia, kuwakumbuka watu waliojitolea mhanga na kukumbatia siku zijazo kwa kuthamini amani.
Rais Xi Jinping pia amezitaka nchi mbalimbali duniani kulinda utaratibu na mfumo wa kimataifa uliojengwa kwenye msingi wa kanuni za katiba ya Umoja wa Mataifa, na kujenga aina mpya ya uhusiano wa kimataifa unaozingatia ushirikiano wa kunufaishana. Ili kufikia lengo hilo ametangaza kuwa China itapunguza wanajeshi wake laki 3.
P yhaa tv coming soon

Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
 


face book ipyana stephen






  Share


















usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos 





Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment