| MASHALI |
Pamoja na
kufanikiwa kumshinda bondia Ibrahim Tamba, mkongwe Thomas Mashali amesema, bwan’mdogo
huyo ni hatari.
Mashali
amekubali kuwamba Tamba ni bondia bora ambaye atasumbua sana hapo baadaye.
Mashali
alimshinda Tamba kwa pointi katika pambano lao la raundi 10 lililopigwa
juzi kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na ushindi huo, Mashali alikiona cha moto ikiwa ni pamoja na kupasuliwa
jicho na Tamba ambaye alikuwa akipambana bila kuchoka.
“Tamba
ni bondia mgumu na alijiandaa sana, utaona nilifanya kila linalowezekana lakini
aliendelea kupambana.
“Nimeshinda
kihalali, kila mmoja ameona. Lakini lazima nikubali bwana mdogo alitoa upinzani
mkali,” alisema.
Mashali amesema Tamba anaweza kuwa mmoja wa mabondia bora kabisa kama atajiendeleza vizuri katika mchezo huo.
P yhaa tv coming soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

0 comments:
Post a Comment